Friday, June 28, 2013

How far have you gone with it?

Can you believe that it’s almost the middle of 2013 already?

If you’re anything like me you started out this year with big dreams and intentions to deliver on some signficant goals in your life.


However along the way to reaching ones goals often comes a lot of distractions and challenges to get you off track. But how far have you gone?.

How did you make it?.

Why did you fail?
 What is your advise to others?

Thursday, May 16, 2013

jitambue Ya Chris Mauki....JINSI GANI YA KUWA NA MAWASILIANO YALIYO BORA NA YENYE UFANISI




Mawasiliano bora  ni muhimu sana kwa mafanikio yetu katika nyanja mbalimbali.  Kama hatuna mawasiliano yaliyobora au hatuwezi kuwasiliana inavyotakiwa basi itakuwa ngumu kwa watu wengine kutusaidia katika kile tunachokihitaji.  Mawasiliano yasiyo bora au kushindwa kuwasiliana vema kunadumaza na mara nyingine kuua kabisa mahusiano baina yetu na wengine.  Kwa  maana hii basi hauna budi kuzingatia sana maelezo na ushauri kutoka katika mada hii na kuyaweka maelezo haya katika matendo ili yakusaidie maishani.

Vitu vya kuzingatia.
  1. Yatazame au yachukulie mazungumzo yako na wale unaohusiana nao kama majadiliano ya kawaida tu na sio mashindano.
Hii itakusaidia kuwa na mahusiano na mawasiliano bora na wengine hususani pale utakapoyaona yale mnayozungumza mara kwa mara kama majadiliano na siyo mashindano. Majadiliano ni mazungumzo yenye kusudi la kufikia suluhisho au muafaka fulani.  Ni mazungumzo ambayo yanapotumika nia yake siyo kumuumiza, kumuumbua mtu bali kutoa nafasi kwa pande zote kufikia matokeo bora. 

Mazungumzo ya yenye ushindani ni yale yenye nia ya kuumiza, kuumbua, kuaibisha, na kudharaulisha, na ambayo nia yake ni kumuonyesha mshindi na aliyeshindwa mwishoni mwa mazungumzo hayo.

Wale wenye tabia ya kuzungumza kiushindani huyachukulia mazungumzo kamanafasi ya kuonyesha ubabe au kunyanyasa wengine. Hata kama  yule mnayezungumza naye ana nia ya mashindano, wewe fanya majadiliano ya kawaida ili taratibu uweze kumbadilisha mtazamo wake.
  1. Kuwa msikilizaji makini na hitaji kusikilizwa pia
Kati ya alama za uonyesha kuwa wewe ni mwenye mawasiliano bora ni pamoja na uwezo wa kuwa msikilizaji mzuri.  Wako watu ambao hupenda kuongea tu na sio kusikiliza.  Sambamba na hilo, unatakiwa kuomba na wewe pia usikilizwe vizuri. Muombe yule anayekusikiliza akuache umalize kuongea ndio na yeye aanze kuongea.  Kamwe hamtafikia muafaka wowote ikiwa wote wawili mnaongea kwa wakati  mmoja.
Yafuatayo yatakuwezesha kuwa msikilizaji mzuri
-          Msikilize yule anaeongea kwanza na kumuelewa
-          Fahamu fika kile kinachozungumzwa elewa nia na dhumuni la majadiliano
-          Uliza swali pale unapodhani hujaelewa ili uweze kuelewa vema nia ya mzungumzaji
-          Jaribu kuweka kwa kifupi au kwa muhtasari kile kilichozungumzwa, mweleze anayezungumza unavyojihisi juu ya  alichokuwa akikieleza, na hakikisha  ulimuelewa vema.
-          Eleza unavyofikiri wewe.  Mweleze aliyekuwa anazungumza kamaumekubaliana nae au la, toa sababu za kukubaliana au kutokukubaliana.

  1. Kuwa mzungumzaji mwenye ujasiri.
ujasiri katika mazungumzo huchochea uhalisi na kuaminika katika kile unachokisema.
Zifuatazo ni tabia za mzungumzaji bora;
a)      Tumia sentensi zinazokuelekea wewe zaidi ya sentensi zinazo waelekea wengine. Jilenge wewe zaidi ya kuwalenga wenzako unapozungumza. unapotumia sentensi za “ninyi” au “wewe” mara nyingi unaweza kuonekana usiye na ujasiri, tofauti na pale unapotumia sentensi zenye “mimi”. Unaweza kuonekana pia kama usiye yaamini  maneno yako.
      Sentensi zenye ujasiri na zenye kukulenga wewe binafsi ni kama vile
 “nimefurahi kukuona”
 “Ningependa kuzungumza na wewe”   
“Sijafurahishwa na maneno yako”

b)      Katika  mazungumzo yako tumia zaidi sentensi na siyo maswali. Hii itakuwezesha pia kuonyesha kuwa unaujasiri katika kile  unachokisema na unajiamini  wewe mwenyewe pia.

Mfano wa mazungumzo yakutumia swali: “Hivi ninyi mnamwonaje yule rafiki yetu?”
Badala yake  ungetekiwa kusema “mimi sifurahishwi na matendo ya huyu rafiki yetu”
Au maranyingine baba wa nyumba anapouliza “Hivi mnadhani nani baba humu ndani?” hii huonyesha kutojiamini kwake
“Hivi unafikiri mimi njinga?”
“Hivi jamani  sisi hatupewi huduma?”
Namna nyingine bora zaidi ya kuuliza swali
-          Je waweza kunisaidia tafadhali?
-          Je utakubali kuoana na mimi?
       Namna bora ya kuzungumza katika sentensi
-          nitafurahi sana ikiwa utakubali kuoana namimi.
-          Nitafurahi sana kupata msaada kutoka kwako

c)      Tumia zaidi sentensi zenye “kukiri” na sio sentensi zenye lawama. Sentensi zenye ukiri au kukiri ni zile ambazo anayezungumza anasema kile ambacho angetaka aone kikifanyika au kile ambacho angependa akione kikitendeka.
Kinyume chake ni sentensi zenye lawama; hizi ni zile ambazo mzungumzaji ana sema kile asichotaka, au kile asichokipenda kitokee au kifanyike.
Mfano wa sentensi zenye lawama:
·         Sipendi kabisa vile unavyonichukulia
·         Sipendi kabisa unavyoniingilia katika maongezi

Mfano wa sentesi zenye kukiri; “Ningefurahi kama ungesubiri nimalize kwanza kuongea  halafu na wewe utaongea”

Sentensi zenye lawama huonyesha ukosefu wa ujasiri kwa mzungumzaji,  mbaya zaidi, sentensi hizi hazisaidii chochote katika kubadili tabia ya yule anayeambiwa maana hazionyeshi bayana ni nini kinachotakiwa kufanyika.

Sentensi zenye lawama pia huonyesha wazi tabia yako sugu ya kulaumu, pia huonyesha vitu usivyovipenda tu, na kuvisahau vile vizuri unavyovipenda.  Ni ngumu sana kumsaidia mtu ambaye analaumu usiku na mchana kuwa hapendi hiki, hapendi kile, hataki hiki na wala hataki kile na bado hawezi kusema anapenda au kutaka nini badala yake.  Kwa hali hii watu hawa wanabaki kuwa walaumu mara dufu.

  1. Lugha ya  mwili wako iwe nzuri (Positive Body language)
Lugha ya mwili ni vile tunavyoweza kutumia miili yetu kuonyesha nia zetu.  Mwili ni kiungo muhimu sana cha mawasiliano.  Tafiti zinasema kwamba, hata wakati mtu anazungumza kupitia mdomo, asilimia 60 (sitini) ya ujumbe wake kupitia au kueleweka sio kwa kupitia maneno ya kinywani mwake bali ni kwa kupitia lugha ya mwili wake.  Jambo hili ndilo hutiliwa  mkazo na ule usemi usemao “matendo husungumza zaidi kuliko maneno”

Lugha ya mwili huusisha vitu kama vile; muonekano wa sura (facial impression), mikunjo ya uso, macho yalivyowekwa, kinywa kilivyo tumiwa, pua inavyofanywa wakati wa kuongea, mikono na pozi ya mwili ilivyo wakati wa kuzungumza.
Ni vema kujikumbusha kila wakati kuhusu umuhimu wa lugha ya mwili ili itusaidie kujijua sisi wenyewe na ule ujumbe tunaoutuma.

Hapa nataka kujaribu kueleza baadhi ya maeneo ya lugha ya mwili ambayo yatakusaidia kuweza kubadilika au kujirekebisha katika mchakato mzima wa mawasiliano kupitia mwili wako.

a)      Kutembea kwa hatua za kudunda au kunesa
Kutembea huku kuwasilisha hisia za ujasiri. Tabia hii huweza kuwa ya asili au ya kujifanyisha hususani apale unapodhani kuwa unachofanya ni cha muhimu zaidi na unapoamini kuwa wewe ni bora zaidi. Kutembea kwako kwaweza kuonyesha  kila kinachoendelea akilini mwako.

b)     Kupanda au kushuka, uzito au wepesi wa sauti unapoongea (Tone of voice)
Pale unapojua hauna ugomvi au uadui na yeyote basi sauti yako itakuwa nzuri, na yakiasi cha kusikika na yeyote.  Vituo vyako na misemo yako itakuwa ya kawaida na yenye uwiano. Pale unapohisi hofu, au kuwepo kwa wabaya wako, mara nyingi sauti yako huwa chini na isiyo na ujasiri.
Unashauriwa kwa hali yoyote ujitahidi kuzungumza kwa sauti ya kati, isiyo chinisana wala juu sana.
c)      Mavazi sahihi
Unapohisi una nafasi fulani katika jamii au sehemu fulani utajikuta unajali sana  suala la kuvaa kwako. Mavazi huweza kuzungumza nia ya moyo na huweza kuonyesha picha mbaya au nzuri kwa wanao kutazama. Mavazi ya aina fulani huweza kukupa tafsiri mbaya kwa watu tofauti na vile ulivyo kihalisia, au kwa upande mwingine mavazi mengine yamefanya wengine kuonekana kama vile ni wa maana sana na wakutegemewa wakati uhalisi haukuwa hivyo
d)     Pozi zuri la mwili
Kuketi au kutembea katika mwili ulionyooka huonyesha ujasiri.  Hii inamaana kifua kinakuwa mbele na tumbo ndani kidogo.  Hata askari waliojasiri huwa hulazimika kuwa katika pozi hili.  Pozi zuri ni ishara ya ukakamavu na afya njema pia.
e)      Muonekano wa macho
Muonekano wetu machoni huweza huonyesha hofu, aibu au ujasiri, hususani tunapokutwa katika maeneo au matukio ambayo hatukutarajia. Muonekano wa macho huthibitisha ukweli au uongo wa kile tunachozungumza.  Muonekano wa macho yetu huweza pia kuthibitisha kumaanisha au kutokumaanisha, uhakika au kutokuwa na uhakika katika kile tunachokizungumza. Wako wengine wasioweza kamwe kuwatazama machoni wale wanaowahofia au kuwaogopa. 
f)       Ukaribu au mgusano
Tabia ya kujitenga na wengine huweza kumaanisha kujikweza au kukosa ujasiri.  Jaribu kuwa karibu na wengine zaidi kadri utamaduni wa jamii uliyopo unavyokuruhusu.  Kama kukumbatia kunaruhusiwa katika jamii yako fanya hivo, kama kushika mkono ndio kunakoruhusiwa basi hakikisha unafanya hivyo, mara kwa mara. Mgusano wa mwili unamaana kubwa sana katika kuongeza ukaribu baina ya watu.
g)      Ishara za mwili (gestures)
Tumia ishara unapoongea. Mfano tumia mikono, tumia kichwa na macho kusisitiza unachoongea.  Kuongea tu kwa madomo pasipo kiungo chochote cha mwili, hufanya mazungumzo yako huwa butu sana.  Ishara za mwili tunazitumia kusisitiza au kuthibitisha tunachokiongea.  Ishara hizi za mwili zitumike taratibu, zisizidishwe sana maana na zaweza kuwabughudhi wengine.


Chris Mauki
Social, Relationship and Counseling Psychologist
E-mail: chrismauki57@gmail.com

Wednesday, February 13, 2013

ZAWADI YANGU YA VALENTINE'S DAY KWENU



NINI MAANA YA URAFIKI.
Kwa ufupi na kwa maneno rahisi; Urafiki ni uhusiano mzuri kati ya watu wawili au zaidi.
Kwa kufafanua zaidi, Urafiki ni uamuzi wa binafsi wa mtu, kuchagua uhusiano wa karibu na mtu mwingine kutokana na misimamo na haja za moyo wake. Urafiki ni kujitoa au kuji-commit (commitment) kwa mwengine au wengine kutokana na uamuzi wa binafsi wa moyoni mwa mtu huyo kulingana na misimamo, machaguo na haja za moyo wake katika maisha yake.

KWANINI TUNAHITAJI MARAFIKI?
1.  Kujaza hitaji la binadamu la kupendwa na kupenda. (Math 22:37-39)
Kila mtu ameumbwa na haja ya kupenda kutambulika na kuthaminika. Urafiki unatupa kujisikia kupendwa na kujaliwa na kutabulika. Usipokuwa na marafiki, utasikisikia kutothaminika.
2.  Kujaza hitaji la kibinadamu la kushirikiana, kusaidiana na kuchangamana. (Mhu 4:9-10)
Hakuna mtu ameumbwa kujitosheleza mwenyewe tu kwa mahitaji ya kimwili kiroho na kiakili. Hakuna mtu anayejua kila kitu wala hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu. Ndio maana Biblia inasema tunafahamu kwa sehemu tu (1Kor 13:9). Mtu huwezi kuishi kama kisiwa peke yake. Tumeumbwa na mapungufu ambayo yanaweza kujazwa na watu wengine.kwaababu hiyo, tunahitajiana. Urafiki unatupa kuchangamana na kushirikiana maisha yetu na wengine. Kuna wakati wa kila jambo chini ya jua. Maisha yamejaa nyakati za furaha na taabu pia. Marafiki wanatusaidia kuwa nasi nyakati zote.
3.  Kuweza kuwafahamu watu na kujifahamu mwenyewe.
Kuchangamana na watu katika urafiki na ushirika mbalimbali, kunatupa kuwafahamu watu wengine tabia zao, mienendo yao, fikra zao, maisha yao n.k. Kuwajua watu kunakuwezesha kujijua na wewe pia, kwamba moyo ukoje (haupendi mambo/vitu fulani na unapenda mambo gani)
4.  Kujifunza na kujiendeleza kitabia, kiakili na kiroho.
Ni marafiki wanaoweza kutusaidia kuwa watu wazuri zaidi kitabia kwa kutubadilisha mienendo isiyofaa. Ni marafiki wanaotufundisha maarifa na elimu mbaimbali. Pia ni marafiki wanaoweza kutusaidia kukua kiroho na kumjua Mungu zaidi.
5.      Kwa ajili ya kupata mwenzi wa maisha. (Mwa 2:8,18)
Kati ya watu tunaowafahamu na kukutana nao katika maisha ya kila siku, Mungu atakupa mwenzi wa maisha (mume au mke). Ni muhimu kufahamiana vizuri kabla ya kuingia katika nadhiri za kuoana, kwasababu maisha mazuri ya furaha na amani, huwafuata watu wanaoendana, wanaoelewana na wanaofanana. Urafiki unakupa kuwafahamu watu na kati ya hao, utakutana na mwenzi wako wa maisha.
AINA ZA MARAFIKI

1.         PEER FRIENDS  (Marafiki wa mbali) *Luke 6:14-17
Ni wale marafiki tunaokutana au kushirikiana nao mambo ya kawaida ya kila siku.
2.         CASUAL FRIENDS  (Marafiki wa kawaida) *Luke 10:1,17-20 *Math 10:1-8,;
Ni wale tunaopenda kuwa nao katika vitu tunavyopenda kuvifanya. (Company)
3.                  CLOSE FRIENDS. (Marafiki wa karibu) *Math 17:1-9 *Mith 18:24 *Luk 8:50-51
Ni wale tunaopenda kuwashirikisha siri na mambo yetu ya muhimu sana.‘best friends’.
4.                  INTIMATE FRIENDS. (Marafiki wa moyoni) *Yoh 10:30 *Math 26:36-44
Ni yule mmoja na wapekee ambaye umempa moyo wako wote na maisha yako (mpenzi)
Aweza kuwa - Rafiki Mpenzi, Rafiki Mchumba au Rafiki Mwanandoa.
5.         MENTOR FRIENDS (Marafiki walezi) * Kut 24:12-18  *Kut 33:7-11
Ni wale marafiki waliotutangulia kwa umri au uzoefu au maarifa ya kimaisha na kiroho. Urafiki ulio katikati yenu ni wa kulea, kufunda, kufunza maarifa ya kimaisha na kiroho. (1Tim 1:2)



SIFA NA TABIA ZA MARAFIKI WAZURI
1.   Anakufahamu/Anakujua. (He/She knows you and knows about you.)
Ahafahamu majina yako, historia yako, ndugu zako, matakwa yako, mipango yako, nk.
            2.   Anapenda kuwa nawe (He/She loves your presence)
      Anapenda na anatafuta muda wa kukutana nawe (company).
3.   Anawasiliana nawe (Communicates)
            4.   Anakujali na Anakusaidia (Cares and gets concerned)
      5.   Anakuheshimu na kukuthamini (Respect and Honour)  
      6.   Anakuvumilia/Anachukuliana nawe (Patient and Barerence)
      7.   Anakuwa Mkweli na Mwaminifu (True and Faithful)
      8.   Anakurekebisha na Anakuonya (Corrects and Worns)
      9.   Anajitoa na ni Mtoaji kwako (Sacrifice and Giver)
          10.   Anakuamini na kukutegemea (Trust and Dependance)

         
                         AINA ZA UPENDO.



1.      UPENDO AGAPE - UPENDO WA MUNGU. (Godly Love)  Rum 5:8 Yoh 3:16
Agape ni aina ya upendo wa ki-Mungu, utendao kazi ndani ya mtu pasipo masharti yoyote au
Mfano; Upendo wa Msamaria mwema. (Luka 10:29-37)
Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa ki-Mungu (Agape).
        i.            Hauangalii hali ya mtu ya nje.
      ii.            Hauna masharti yoyote ya kupenda.
    iii.            Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.
    iv.            Hauna mwisho au kikomo cha kupenda.

2.      UPENDO PHILEO – UPENDO WA KIRAFIKI. (Friendship Love)
Phileo (Kiebrania)  ni upendo wa kirafiki. Phileo ni upendo wenye sababu. Kiingereza wanasema ‘congitional love’. Ni upendo wenye sababu. Huu ndio upendo unaokuwepo kati ya marafiki. Yohana 14:21,23. Mithali 8:17
Mfano; Urafiki wa Jonathan na Daudi. (1Samweli 18:1-4)
  Urafiki wa Yesu na Lazaro, Mariam na Martha. (Yohana 11:5, 35-36)


Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa kirafiki (Phileo).
        i.            Unaangalii hali ya mtu ya nje.
      ii.            Una masharti yoyote ya kupenda.
    iii.            Una kiwango au kipimo cha kupenda.
    iv.            Una mwisho au kikomo cha kupenda.

3.                              UPENDO EROS – UPENDO WA KIMAPENZI AU MAHABA. (Romantic/Sexual  Love)
Eros ni upendo wa kimapenzi au kimahaba unaokuwa kati ya watu fulani kusababisha watu hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi (mahaba) kati yao. Kwa utaratibu wa Mungu na jamii zilizo ‘sawa sawa’, Eros ni aina ya upendo unaotakiwa kuwa kati ya watu wenye uhusiano wa ki-ndoa, yaani mtu mke na mume au kati ya watu wanaoelekea katika uhusiano wa ki-ndoa wa mume na mke. (Waefeso 5:25;  Mhubiri 9:8-9; Wimbo Ulio Bora 7:1-10; Wimbo Ulio Bora 4:1-7)
  Mfano;  Upendo wa Yakobo kwa Raheli. *Mwanzo 29:16-20 (10-30)
                Upendo wa Isaka kwa mkewe Rebecca. (Mwa 26:1-11)
  Sifa / Baadhi ya Dalili za Upendo Kimapenzi (mahaba) Eros.
1)      Mvuto kwa Haiba yake na kuchukuliana nayo. (Mwonekano na tabia).
2)      Kukaa mawazoni kwa mtu anayependa. (Kujaa moyoni)
3)      Shauku kubwa ya kuwa pamoja kila wakati. (Kuambatana)
4)      Heshima kubwa kwa mtu apendwae (Utii na Uaminifu)
5)      Kumjali na kumtanguliza mtu apendwae. (Kipaumbele)
6)      Zawadi na gharama kwa mtu apemdwae. (Kujitoa/Sacrifice)
7)      Furaha na Amani kutawala moyoni. (Kuridhika)

4.                              UPENDO STORGE – UPENDO WA KIFAMILIA. (Family Love)
Upendo storge ni upendo wa kifamilia, ni upendo unaotokana na damu moja ya undugu.
Mfano; Upendo wa Musa kwa Mwebrania mwenzake. (Kutoka 2:11-12)
 Upendo wa Baba kwa Mwana mpotevu. (Luka 15:11-32)
Upendo wa kindugu, storge  unafanana kwa sehemu na ule upendo wa ki-Mungu wa agape.
  1. Hauangalii hali ya nje ya mtu.
  2. Hauna masharti ya kupendwa.
  3. Hauna kikomo au mwisho wa kupendwa.

Tofauti yake moja kubwa na upendo wa agape ni kwamba, upendo wa kindugu una kiwango au kipimo cho kupenda. Ndugu wanapendana lakini kwa viwango tofauti; upendo wao haulingani. Tofauti ningine kubwa ni kwamba, kwasababu huu upendo wa kindugu unatokana na binadamu, basi ni lazima hautakosa madhaifu mengi.










NAMNA YA KUPATA MWENZI MZURI WA MAISHA.
(HOW TO FIND/GET A GOOD MARRIAGE PARTNER)
*Mithali 19:14, 21

1.      Mweleze Mungu vizuri, zile haja za moyo wako. (Mwa 2:18)
Mungu anaheshimu sana haja za moo wako ambazo zitakupa wewe furaha ya maisha.
(Mathayo 7:7-11;  Wafilipi 4:6-7 ; Zab 145:17-18) Hii ni kwasababu, Mungu anaheshimu sana matakwa na mahitaji ya watoto wake, maana anapenda kuiona furaha ya watoto wake.
Isa 45:11 ; 1Kor 7:39; Yak :16,  Luk 18:1,  Kol 4:2.

2.      Mwombe Mungu akuonyeshe au akukutanishe na mwenzi wako. (*Yer 33:3)
Kumwomba Mungu kusababisha mazingira ambayo yatawakutanisha na mtatambuana baada ya kupata ufahamu wa Mungu kwamba ‘you belong together’ yaani mnaendana, mnafanana, mnafaana na hivyo mnaweza kuishi pamoja vizuri. Hiyo ndiyo maana halisi ya kufunuliwa au kuonyeshwa. Japo Mung5 anaweza kukupa maono katika ndoto au katika maombi, lakini si lazhma iwe hivyo. Si kila mtu anaweza kupata maono kuhusu mwenzi wake. Soma Efe 1:15-19, Jab 32:,  Isa 43:26,  Isa 45:11

3.      Tengeneza marafiki. (*Mith 18:24, Mith 17:17)
Watu wengi humwomba Mungu kwa uaminifu sana ili wapate mwenzi wa maisha. Lakini wanfanya makosa ya kujifungia katika kisiwa cha upekee. Ni ngumu sana kuOnekana na kujulikana tabia na utu wako wa ndani kama hudachangamana na jumuiya za ma2afiki. MunGu ndiye chanzo cha urafiki. Hat Yesu alikuwa na marafiki wa kiume na waki kike pia. (Yoh 11:5).  Jithidi kufanya marafiki mvalimbali ila mwombe Mungu akupe marafiki wazuri. Mk 5:25 – (30) – 34; inasema, wengi walimgUsa Yesu na kumsUkuma-sukuma, lakini ni mmoja tuambaye atakuwa na mguso wa tofauti katika moyo wako.

ISHARA ZA KUTAMBUA (UPENDO WA) PENZI LA KWELI.
1.      Mtu huyo atakamata umakini wako na atakuvutia (attention).
2.      Atajaa moyoni na mwazoni mwako kuliko kawaida na wengine.
3.      Utatamani sana uwepo wake wakati wote (kuwa naye).
4.      Utapenda kuwasiliana naye mara kwa mara (kama hamko wote).
5.      Utakuwa na moyo wa kumjali, wema, zawadi na kujitoa sana kwa ajili yake.
6.      Utakuwa na heshima ya juu sanA, adabu, uTii na uaminifu sana kwake.
7.      Utakuwa na maneno mazuri, maneno laini, na maneno ya upendo kwake.
8.      Utakuwa na moyo/uwezo wa kumvumilia au kuchukuliana naye vile alivyo.
9.      Utakuwa na hamu ya kumgusa au kumshika kwa upendo (si tamaa).
10.  Utakuwa na moyo na utayari wa kumlinda Na kumhifadhi.
11.  Uhusiano wenu utapendeza mbele za watu wengi (si lazima wote)
12.  Utakuwa na amani na furaha ya ajabu moyoni mwako/mwenu.

Mungu alisema kwa mkono wa Mtume Paulokuuelezea Upendo kwA namna hii;
1 Cor 13 : 4-8(a)
*          Upendo huvumilia/subira  (Love is patient)
*          Upendo hufadhil)/hufania wema (Love is kind)
*          Upendo hauna husuda (Love doesn’t Envy)
*          Upendo haujivuni (Love is not proud)
*          Upendo haukosi adabu (Love is not rude)
*          Upendo hauna ubinafsi (Love is not selfish)
*          Upendo hauna uchungu (Love is not easily angered)
*          Upendo hauhesabu mabaya (Love doesn’t count wrongs)
*          Upendo haufurahii uovu (Love doesn’t rejoice with evil)
*          Upendo hufurahia ukweli (Love rejoices in truth)
*          Upendo unalinda (love always protects)
*          Upendo huamini yote (Love always trusts)
*          Upendo hutumaini (Love always hopes)
*          Upendo hustahimili (Love always perseveres)

5.  Omba ushauri kwa watu wanaokujua/wanaomjua huyo umpendaye.
2Kor 13:1; Zab 73:24; Mith 15:22
Ushauri kutoka kwa watu werevu wanaomjua Mungu na wanaowajua ninyi wawili utakuhibitishia kwamba ulichsikia mooni juu ya huyo mtu ni sahihi. Mashauri ya watu yanaweza kukusaidia kufanya maamuzi magumu nay a muhimu.
(Math 18:16;   1Tim 5:19;   Ebr 10:28; Fil 4:6-7, Kol 3:15 na Isa 55:12

6.  Mwendee na Useme naye kwa hekima.   (*Wimbo 3:1-4)
Baada ya maombi na subira, Mungu akuongoze kusema naye kwa wakati utakaoongozwa na Mungu. Uwe jasiri na muwazi. Lakini usemi wako uwe wa kawaida (simple). Usichague maneno magumu wala misamiati wala mafumbo. Uwe wazi na wa kawaida.

7.    Thibitisha uhusiano wako/wenu (kiofisi).  (*Wimbo 3:4)
Baada ya kuongea na kulitafakari pamoja kwa muda mtakaoona unatosha au unafaa, ni muhimu sana sasa mpelekane mbele, katika mamlaka zenu za kifamilia na kikanisa. Uhusiano mzuri usiwe wa mafichoni. Tunaona huyu mpenzi katika kitabu cha Wimbo anasema, anataka kumtafuta mpenzi wake, amshike mkono, wapelekane kwa wazazi. Huo ndio utaratibu mzuri kibiblia. Familia na kanisa watawasaidia kufuata taratibu za kiutamaduni na kiroho ili mhalalishwe kuwa mume na mke. Ndipo ndugu na marafiki mtawashirikisha mipango yote ili kuandaa harusi na maka